Ephesians 2:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili katika ulimwengu ujao apate kuonesha wingi wa neema yake isiyolinganishwa, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alifanya hivi ili wema wake kwetu sisi tulio wa Kristo Yesu uweze kuonesha nyakati zote zijazo utajiri wa ajabu wa neema yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndivyo alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana siku zitakazokuja anataka kuonyesha, magawio yake yanavyokuwa mengi, yasipimike akituendea kwa utu tu katika Kristo Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifanya vile kusudi aonyeshe kwa vizazi vyote vitakavyokuja neema yake kubwa ya ajabu kwa njia ya wema wake katika kuungana kwetu na Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.