Ephesians 3:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
sawasawa na kusudi lake la milele alilolitimiza katika Al-Masihi Isa Bwana wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii inaendana na mpango aliokuwa nao Mungu tangu mwanzo wa nyakati. Alitekeleza mpango wake kupitia Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
sawasawa na kusudi lake la milele katika Al-Masihi Isa Bwana wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenyewe aliviweka hivyo kale kabisa moyoni mwake, vitimie katika Kristo Yesu, Bwana wetu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu amefanya hivi kufuatana na kusudi lake la milele alilofanya kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.