Ephesians 3:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kipawa cha neema ya Mungu, nilifanywa mtumishi wa kuihubiri Habari Njema. Alinipa neema hiyo kwa nguvu zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Habari Njema kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Injili hiyo ambayo nilifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndio, niutumikiao nami kwa hivyo, Mungu alivyonigawia kipaji changu, nilichopewa hapo, niliposhindwa na nguvu zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimewekwa kuwa mutumishi wa Habari Njema kwa njia ya zawadi Mungu aliyonipatia kutokana na uwezo wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake.