Ephesians 4:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana Isa, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, mimi niliye mfungwa kwa ajili ya Bwana nawasihi mwishi kwa jinsi inavyowapasa watu wa Mungu, kwa sababu aliwachagua muwe wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana Isa, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mimi niliye mfungwa kwa kuwa namtumikia Bwana, nawasihi muishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Mimi niliyefungwa kwa ajili ya Bwana nawaonya ninyi, mfanye mwenendo unaopatana na wito, mlioitiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hivi basi, mimi ninayekuwa mufungwa kwa sababu ninamutumikia Bwana, ninawasihi muishi sawa inavyostahili kufuatana na mwito Mungu aliowatolea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,