Ephesians 4:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hadi sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima, kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kazi hii inabidi iendelee hadi wote tutakapounganishwa pamoja katika lile tunaloliamini na tunalolijua kuhusu Mwana wa Mungu. Lengo letu ni kufanana na mtu mzima aliyekomaa na kuwa kama Kristo tukiufikia ukamilifu wake wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu, na kuwa watu wazima kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mpaka sisi sote tutakapofikia kuwa mmoja wa kumtegemea na wa kumtambua Mwana wa Mungu; huko ndiko kukua kwenyewe na kuutimiza umri unaoweza kuutambua wingi wote wa vipaji vya Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi, sisi wote tutafikia umoja wa imani yetu na wa kumujua kabisa Mwana wa Mungu; tutapata kukomaa na kufikia kipimo cha utimilifu wa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
hatta wote tutakapoufikia umoja wa imani, na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, tuwe watu wakamilifu, hatta cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;