Ephesians 4:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho, na kwa ujanja na hila za watu katika njama zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo tutakapokuwa si kama watoto wachanga. Hatutakuwa watu ambao nyakati zote hubadilika kama meli inayochukuliwa na mawimbi huku na kule. Hatutaweza kuathiriwa na fundisho lolote jipya tutakalosikia kutoka kwa watu wanaojaribu kutudanganya. Hao ni wale wanaoweka mipango ya ujanja na kutumia kila aina ya mbinu kuwadanganya wengine waifuate njia iliyopotoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu, ili wawapotoshe wengine kwa hila.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo hatutakuwa tena wachanga wanaochukuliwa kama mawimbi na kupelekwa huko na huko na mafunzo ya watu yanayogeukageuka kama upepo, maana ni ya uwongo na ya udanganyi wa watu wanaotaka kutupoteza kwa werevu mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukipeperushwa na kuvutwa na mafundisho ya kila aina yanayoletwa na watu wanaodanganya wengine na kuwapotosha kwa mayele yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;