Ephesians 4:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tena usimhuzunishe Roho Mtakatifu. Mungu alikupa Roho Mtakatifu kama uthibitisho kwamba wewe ni wake na kwamba atakulinda hadi siku atakapokufanya uwe huru kabisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba ninyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa mhuri hata siku ya ukombozi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msimsikitishe Roho Mtakatifu wa Mungu! Kwani ndiye, mliyepewa kuwa muhuri yenu ya siku ya ukombozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musihuzunishe Roho Mutakatifu wa Mungu; kwa maana Roho ni kitambulisho kilichowekwa juu yenu kwa kuhakikisha kwamba ninyi ni watu wake mpaka siku Mungu atakapowakomboa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.