Ephesians 4:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu na hasira, makelele na masingizio, pamoja na kila aina ya uovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Usiwe na uchungu, wala kukasirika. Kamwe usiongee kwa hasira au kusema chochote ili uwaumize wengine. Usifanye chochote kilicho kiovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele, matusi! Achaneni na kila uovu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matusi yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uchungu wo wote na mifundo ya mioyo na makali na mateto na matusi na yaondoke kwenu pamoja na uovu wote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutupilie mbali nanyi nia zote za uadui, chuki, kasirani, fujo na masingizio. Mutupilie mbali ubaya wa kila namna!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Uchungu wote na hasira na ghadhabu na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na killa ubaya;