Ephesians 4:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwe mwema na mpendane ninyi kwa ninyi. Msameheane ninyi kwa ninyi kama Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mwenyezi Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwendeane kwa utu na kwa upole, mkiacha kulipishana, kama Mungu naye alivyoacha kuwalipisha ninyi kwa kuwa wake Kristo!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutendeane wema ninyi kwa ninyi; musameheane kama Mungu alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi.