Ephesians 5:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
apate kujiletea jumuiya tukufu isiyo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na isiyo na hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kristo alikufa ili aweze kujiletea mwenyewe kanisa lililo kama bibi harusi katika uzuri wake wote. Alikufa ili kanisa liweze kuwa takatifu na lisilo na dosari, lisilokuwa na uovu au dhambi au chochote kilicho kibaya ndani yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
apate kujiletea jumuiya tukufu isilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na isilo na hatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na dosari wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, alivyotaka kujitengenezea mwenyewe wateule wenye tukuzo hilo la kwamba: Hawanalo doa wala kunjo wala lo lote lifananalo nayo yaliyo hivyo, maana ndio watakatifu pasipo kilema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitaka hivi kujipatia yeye mwenyewe kanisa tukufu na takatifu, lisilokuwa na taka wala kikunjo wala kilema chochote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.