Ephesians 5:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kila mmoja wenu anapaswa kumpenda mkewe kama anavyojipenda mwenyewe. Na mke anapaswa kumheshimu mume wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yanawahusu nyinyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hata ninyi kila mmoja wenu na ampende mkewe, kama anavyojipenda mwenyewe! Lakini mke amche mumewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa hivi, kwa ngambo yenu vilevile, kila mume anapaswa kumupenda muke wake kama vile anavyojipenda, na kila muke anapaswa kuheshimu mume wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe.