Ephesians 5:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana Isa. Nendeni kama watoto wa nuru
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo zamani mlijaa giza, lakini sasa mmejaa nuru katika Bwana. Hivyo ishini kama watoto wa nuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana Isa. Enendeni kama watoto wa nuru
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zamani nyinyi mlikuwa gizani, lakini sasa nyinyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kale mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa mwanga kwa kuwa naye Bwana. Mwendelee, kama iwapasavyo wana wa mwanga!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamani muliishi katika giza, lakini sasa, kwa kuungana kwenu na Bwana, munaishi katika mwangaza. Muishi kama watoto wa mwangaza,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru;