Ephesians 6:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja, nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo sababu mnahitaji silaha zote za Mungu. Ili siku ya uovu, mweze kusimama imara. Na mtakapomaliza mapigano yote, mtaendelea kusimama.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mwenyezi Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo yashikeni mata ya Kimungu yote, mweze kusimama penye mapigano, siku mbaya itakapokuwapo, mpate kuyashinda mabaya yote mkiwa mmesimama vivyo hivyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo sasa mutwae silaha zote Mungu anazowapatia. Kwa njia hii mutaweza kushinda adui yenu siku mbaya itakapowafikia. Nanyi mutakapokwisha kumaliza mapigano, mutaweza kusimama imara.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kutimiza yote kusimama.