Ephesians 6:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana Isa, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Namtuma kwenu Tikiko, ndugu yetu mpendwa na msaidizi mwaminifu katika kazi ya Bwana. Atawaeleza kila kitu kinachonipata. Kisha mtaelewa jinsi nilivyo na ninachofanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana Isa, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ili nanyi pia mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kusudi mpate kujua nanyi, mambo yangu yalivyo, nami mwenyewe nilivyo, yote atawasimulia Tikiko aliye ndugu yetu mpendwa na mtumishi mwelekevu wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tikiko, ndugu yetu mupendwa na mutumishi mwaminifu wa Bwana atawapasha habari zangu zote, kusudi mupate kujua kama mimi ni katika hali gani na namna kazi inavyoendelea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote;