Ephesians 6:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na kutetemeka; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa unyofu wa moyo, kama vile mnavyomtii Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watumwa, watiini bwana zenu hapa duniani kwa hofu na heshima. Na fanyeni hivi kwa moyo ulio wa kweli, kama mnavyomtii Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na kutetemeka; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba mnamtii Kristo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na kutetemeka; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi watumwa, kama mnavyomtii Kristo, watiini nao mabwana zenu wa nchini kwa kuwaogopa na kutetemeka, mkilishika mioyoni mwenu lile Neno moja tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi watumwa, mutii wabwana wenu kwa woga na kutetemeka na kwa moyo wa ukweli kama vile munavyomutumikia Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,