Ephesians 6:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mngemtumikia, wala si wanadamu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fanyeni kazi zenu, na mfurahie kuzifanya. Fanyeni kana kwamba mnamtumikia Bwana, siyo tu bwana wa duniani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana Isa na si wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tumikeni na kuuitikia utumishi, kama sio watu, mnaowatumikia, ila kama ni Bwana, mmtumikiaye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufanye kazi yenu ya utumwa kwa moyo mwema, kama vile wenye kumutumikia Bwana, wala si watu tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa nia njema mkimtumikia Bwana wala si mwana Adamu: