Ephesians 6:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkijua kwamba Bwana Isa atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, awe mtumwa au mtu huru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kumbukeni kwamba Bwana atampa kila mmoja zawadi kwa kufanya vema. Kila mmoja, mtumwa au aliye huru, atapata zawadi kwa mambo mema aliyotenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lo lote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkijua kwamba Bwana Isa atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana awe ni mtumwa au ni mtu huru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mjue: kila mtu akifanya kazi njema yo yote atalipwa naye Bwana, akiwa mtumwa, au akiwa mwungwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukumbuke kwamba Bwana atalipa kila mutu sawa na matendo yake mema, akiwa huru au mutumwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkijua ya kuwa killa neno jema atendalo mtu, atapewa lilo hilo na Bwana, akiwa ni mtumwa, au akiwa ni huru.