Esther 1:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya saba ya karamu hiyo, mfalme Ahasuero, akiwa amejaa furaha kutokana na divai aliyokuwa amekunywa, aliwaita matowashi saba waliomhudumia yeye binafsi: Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba, wakati Mfalme Ahasuero alikuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba waliokuwa wakimhudumia, yaani Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya saba ya karamu hiyo, mfalme Ahasuero, akiwa amejaa furaha kutokana na divai aliyokuwa amekunywa, aliwaita matowashi saba waliomhudumia yeye binafsi: Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku ya saba, wakati Mfalme Ahusuero alipokuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba ambao walikuwa wakimhudumia, yaani, Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya saba, wakati Mfalme Ahasuero alikuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba waliokuwa wakimhudumia, yaani, Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya saba, moyo wa mfalme ulipochangamshwa na mvinyo, akawaambia akina Mehumani, Bizita, Harbona, Bigita, Abagita, zetari, na Karkasi, watumishi wake saba wa nyumbani waliomtumikia mfalme Ahaswerosi mwenyewe,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya saba ya karamu hiyo, mufalme Ahasuero akiwa amejaa furaha kutokana na divai aliyokuwa amekunywa, akawaita matowashi saba waliomutumikia yeye mwenyewe: Mehumani, Bizita, Harbona, Bigita, Abagita, Zetari na Karkasi.