Esther 1:11 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwaamuru hao wamlete kwake malkia Vashti, akiwa amevaa taji yake ya kimalkia. Malkia huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, hivyo mfalme alitaka kuwaonesha wageni wake na viongozi uzuri wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aoneshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri kumtazama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwaamuru hao wamlete kwake malkia Vashti, akiwa amevaa taji yake ya kimalkia. Malkia huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, hivyo mfalme alitaka kuwaonesha wageni wake na viongozi uzuri wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aonyeshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri wa kupendeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aonyeshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri wa kupendeza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wamlete Wasti mkewe mfalme, amtokee mfalme na kuvaa kilemba cha kifalme, awaonyeshe watu wote nao wakuu uzuri wake, kwani alikuwa kweli mwenye sura nzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaamuru hao wamuletee malkia Vashiti, akiwa amevaa taji yake ya kimalkia. Malkia yule alikuwa na sura nzuri sana, hivyo mufalme alitaka kuwaonyesha wageni wake na viongozi uzuri wake.