Esther 1:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini matowashi hao walipomweleza malkia amri ya mfalme, Vashti alikataa kutii. Jambo hilo lilimwudhi sana mfalme, akawa anawaka hasira moyoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika, na hasira yake ikawaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini matowashi hao walipomweleza malkia amri ya mfalme, Vashti alikataa kutii. Jambo hilo lilimwudhi sana mfalme, akawa anawaka hasira moyoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika na hasira ikawaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika, na hasira yake ikawaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Wasti, mkewe mfalme, akakataa kuja kwa ile amri, mfalme aliyompelekea kwa vinywa vya wale watumishi wa nyumbani. Ndipo, mfalme alipokasirika sana, makali yake yakawaka moto moyoni mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Vashiti akakataa kufika kwa amri mufalme aliyotoa kwa njia ya matowashi. Kwa hiyo, mufalme akakasirika sana na hasira yake ikawaka.