Esther 1:16 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Memukani akamwambia mfalme na viongozi wake, “Licha ya kumkosea mfalme, malkia Vashti amewakosea viongozi na kila mtu katika mikoa ya mfalme Ahasuero!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahasuero.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na maakida, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na maakida wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Memukani akamwambia mfalme na viongozi wake, “Licha ya kumkosea mfalme, malkia Vashti amewakosea viongozi na kila mtu katika mikoa ya mfalme Ahasuero!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahusuero.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahasuero.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Memukani akasema mbele ya mfalme na mbele ya hao wakuu: Siye mfalme peke yake, Wasti, mkewe mfalme, aliyemkosea, ila amewakosea nao wakuu wote na watu wote pia walioko katika majimbo ya mfalme Ahaswerosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na maakida, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na maakida wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Memukani akamwambia mufalme na viongozi wake: “Zaidi ya kumukosea mufalme, malkia Vashiti amewakosea viongozi na kila mutu katika majimbo ya mufalme Ahasuero!