Esther 1:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tendo hili la malkia Vashti litajulikana na wanawake wote, nao watawadharau waume zao, wakisema: ‘Mfalme Ahasuero aliamuru malkia Vashti aje kwake, lakini yeye akakataa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahasuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana tendo hilo la malkia litajulikana na wanawake wote, hata waume zao watadharauliwa machoni pao, itakaponenwa ya kuwa mfalme Ahasuero aliamuru Vashti, malkia, aletwe mbele yake, bali hakuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tendo hili la malkia Vashti litajulikana na wanawake wote, nao watawadharau waume zao, wakisema: ‘Mfalme Ahasuero aliamuru malkia Vashti aje kwake, lakini yeye akakataa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahusuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahasuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani jambo hili la mkewe mfalme litatoka, lifike kwa wanawake wote, liwabeue bwana zao machoni pao, maana watasema: Mfalme Ahaswerosi aliagiza kumleta Wasti, mkewe mfalme, aje usoni pake, naye hakuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana tendo hilo la malkia litajulikana na wanawake wote, hata waume zao watadharauliwa machoni pao, itakaponenwa ya kuwa mfalme Ahasuero aliamuru Vashti, malkia, aletwe mbele yake, bali hakuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tendo hili la malkia Vashiti litajulikana na wanawake wote, nao watawazarau waume zao, wakisema: ‘Mufalme Ahasuero aliamuru malkia Vashiti akuje kwake, lakini yeye akakataa.’