Esther 1:18 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Leo hii, mabibi wa Persia na Media ambao wamesikia alivyofanya malkia Vashti, watakuwa wanawaeleza viongozi wako; hivyo dharau na chuki vitajaa kila mahali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya leo, wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia kuhusu tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwa na mwisho wa dharau na ugomvi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata na leo hivi mabibi wastahiki wa Uajemi na Umedi waliokwisha kuzisikia habari za tendo lake malkia watawaambia vivi hivi maakida wote wa mfalme. Hivyo kutatokea dharau nyingi na ghadhabu tele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Leo hii, mabibi wa Persia na Media ambao wamesikia alivyofanya malkia Vashti, watakuwa wanawaeleza viongozi wako; hivyo dharau na chuki vitajaa kila mahali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Leo hivi wake wakuu wa Wapersia na wa Wamedia waliolisikia hilo jambo la mkewe mfalme watalisimulia wakuu wote wa mfalme; ndipo, yatakapokuwa mabezo na mateto ya kutosha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata na leo hivi mabibi wastahiki wa Uajemi na Umedi waliokwisha kuzisikia habari za tendo lake malkia watawaambia vivi hivi maakida wote wa mfalme. Hivyo kutatokea dharau nyingi na ghadhabu tele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Leo hii, wanawake wa Persia na Media ambao wamesikia jinsi malkia Vashiti alivyofanya, watakuwa wanawaelezea viongozi wako; hivyo mazarau na chuki vitajaa kila pahali.