Esther 1:19 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ukipenda, ewe mfalme, toa amri rasmi Vashti asije tena mbele yako. Amri hiyo na iandikwe katika sheria za Persia na Media, ili isiweze kubadilishwa. Kisha, cheo chake cha umalkia, apewe mwanamke mwingine anayestahili zaidi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitabadilika, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahasuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kuliko yeye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ukipenda, ewe mfalme, toa amri rasmi Vashti asije tena mbele yako. Amri hiyo na iandikwe katika sheria za Persia na Media, ili isiweze kubadilishwa. Kisha, cheo chake cha umalkia, apewe mwanamke mwingine anayestahili zaidi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitakaa ibadilike, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahusuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kuliko yeye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitabadilika, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahasuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kumliko yeye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akiyaona kuwa mema, na kutoke kwake amri ya kifalme, iandikwe katika amri za Wapersia na za Wamedia, isitanguke tena, kwamba: Wasti asitokee tena usoni pa mfalme Ahaswerosi, nao utukufu wake wa kifalme mfalme na ampe mwenzake aliye mwema kuliko yey.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ikikupendeza, ewe mufalme, toa amri kwamba Vashiti asikuje tena mbele yako. Amri hiyo iandikwe katika sheria za Persia na Media, kusudi isiweze kubadilishwa. Kisha, cheo chake cha umalkia, kipewe kwa mwanamuke mwingine anayekuwa bora zaidi kuliko yeye.