Esther 1:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wake, mfalme Ahasuero aliwaandalia karamu viongozi na watumishi wake wa serikali, wakuu wa majeshi ya Persia na Media, watu maarufu na wakuu wa mikoa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wake, mfalme Ahasuero aliwaandalia karamu viongozi na watumishi wake wa serikali, wakuu wa majeshi ya Persia na Media, watu maarufu na wakuu wa mikoa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
katika mwaka wa tatu wa ufalme wake ndipo, alipowafanyia wakuu wake wote pamoja na watumishi wake karamu kubwa. Wakawako mbele yake wakuu wa vikosi vya Persia nao vya Media, hata wenye macheo na wakuu wa majimbo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mwaka wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi, watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, mufalme Ahasuero akaandaa karamu kwa ajili ya viongozi na watumishi wake wa serikali, wakubwa wa majeshi ya Persia na Media, watu wenye heshima na wakubwa wa majimbo.