Esther 1:4 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kwa muda wa miezi sita, Ahasuero akaonesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na fahari ya utawala wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa muda wa siku mia moja na themanini mfalme alionesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaonyesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana siku mia na themanini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kwa muda wa miezi sita, Ahasuero akaonesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na fahari ya utawala wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa siku zote 180 mfalme alionyesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa siku zote 180 mfalme alionyesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaonyesha mali na malimbiko ya ufalme wake nayo marembo na utukufu wake mwingi siku nyingi, yaani siku 180.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaonyesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana siku mia na themanini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kwa muda wa miezi sita, Ahasuero akaonyesha utajiri wa ufalme wake mutukufu, na sifa ya utawala wake.