Esther 1:5 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Muda huo ulipomalizika, mfalme aliwaandalia karamu watu wote wa mji mkuu wa Susa, wakubwa kwa wadogo. Karamu hiyo iliyochukua muda wa siku saba, ilifanyika uani, katika bustani ya ikulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hizo zilipopita, mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliokuwa katika ngome ya mji wa Shushani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku hizo zilipotimia, mfalme akawafanyia karamu watu wote waliokuwapo huko Shushani ngomeni, wakubwa kwa wadogo, muda wa siku saba, katika behewa la bustani ya ngome ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Muda huo ulipomalizika, mfalme aliwaandalia karamu watu wote wa mji mkuu wa Susa, wakubwa kwa wadogo. Karamu hiyo iliyochukua muda wa siku saba, ilifanyika uani, katika bustani ya ikulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hizo zilipopita, ndipo mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, ambao walikuwa katika ngome ya mji wa Shushani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hizo zilipopita, mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliokuwa katika ngome ya mji wa Shushani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo zilipokwisha kupita, mfalme akawafanyia watu wote pia waliopatikana mle Susani penye jumba lake, wakubwa kwa wadogo, karamu ya siku saba uani penye bustani ya jumba la mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku hizo zilipotimia, mfalme akawafanyia karamu watu wote waliokuwapo huko Shushani ngomeni, wakubwa kwa wadogo, muda wa siku saba, katika behewa la bustani ya ngome ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muda ule ulipomalizika, mufalme aliandaa karamu kwa ajili ya watu wote wa muji mukubwa wa Susani, wakubwa kwa wadogo. Karamu hiyo iliyokamata muda wa siku saba, ilifanyika ndani ya kiwanja, katika bustani ya nyumba ya kifalme.