Esther 1:6 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali hapo palikuwa pamepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya buluu. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za fedha kwa kamba za kitani safi za zambarau, na kuninginizwa kwenye nguzo za marumaru. Makochi ya dhahabu na fedha yalikuwa yamewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa vijiwe vya rangi, marumaru, lulumizi na mawe ya thamani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bustani ilikuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marumaru. Kulikuwa na viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marumaru, lulumizi na mawe mengine ya thamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na mapazia ya bafta, nyeupe na samawi, yamefungiwa kamba za kitani safi za rangi ya zambarau kwa pete za fedha na nguzo za marumaru; pia na vitanda vilikuwa vya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marumaru, mawe mekundu, na meupe, na ya manjano, na meusi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali hapo palikuwa pamepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya buluu. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za fedha kwa kamba za kitani safi za zambarau, na kuning'inizwa kwenye nguzo za marumaru. Makochi ya dhahabu na fedha yalikuwa yamewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa vijiwe vya rangi, marumaru, lulumizi na mawe ya thamani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bustani iliyokuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marmar. Kulikuwepo viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marmar, lulumizi na mawe mengine ya thamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bustani ilikuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marmar. Kulikuwepo viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marmar, lulumizi na mawe mengine ya thamani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mazulia meupe na meusi mazuri mno yalikuwa yamefungwa kwa kamba za pamba nyeupe na nyekundu katika pete za fedha penye nguzo za mawe meupe. Nayo magodoro ya kukalia yaliyofumwa kwa nyuzi za dhahabu na za fedha yalikuwa yametandikwa sakafuni palipotengenezwa kwa mawe mekundu na meupe na ya manjano na meusi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na mapazia ya bafta, nyeupe na samawi, yamefungiwa kamba za kitani safi za rangi ya zambarau kwa pete za fedha na nguzo za marumaru; pia na vitanda vilikuwa vya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marumaru, mawe mekundu, na meupe, na ya manjano, na meusi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pale kulikuwa kumepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya samawi. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za feza kwa kamba za kitani safi nyekundu-nyeusi, na kutundikwa kwenye nguzo za mawe ya marimari. Viti vya zahabu na feza vilikuwa vimewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi ya marimari, nyekundu, nyeusi, manjano na nyeusi.