Esther 1:8 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mtu alikunywa akashiba; mfalme alikuwa ametoa maagizo kwa watumishi wa ikulu wamhudumie kila mtu kadiri ya mahitaji yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote kugawa mvinyo kila mtu kwa jinsi alivyotaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kunywa kulikuwa kama ilivyoamriwa, bila sharti; maana ndivyo mfalme alivyowaagiza watumishi-wa-nyumbani, kila mtu afanye apendavyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mtu alikunywa akashiba; mfalme alikuwa ametoa maagizo kwa watumishi wa ikulu wamhudumie kila mtu kadiri ya mahitaji yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote wa kuhudumu mvinyo kumhudumia kila mtu kwa jinsi alivyotaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote wa kuhudumu mvinyo kumhudumia kila mtu kwa jinsi alivyotaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ilivyoagizwa, watu wakanywa, kama walivyotaka pasipo kushurutishwa; kwani nidvyo, mfalme alivyowaagiza wakuu wote wa nyumbani mwake, waache, kila mtu anywe, kama anavyopendezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kunywa kulikuwa kama ilivyoamriwa, bila sharti; maana ndivyo mfalme alivyowaagiza watumishi-wa-nyumbani, kila mtu afanye apendavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutu alikunywa sawa vile alivyotaka; mufalme alikuwa ametoa maagizo kwa watumishi wa nyumba ya kifalme wamutendee kila mutu kadiri ya mahitaji yake.