Esther 10:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Na kuhusu matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amempandisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Matendo yote ya uwezo wake na ya nguvu zake na habari zote za macheo makuu, mfalme aliyompa Mordekai, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wao Wamedi na Wapersia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matendo yake yote makubwa na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili juu ya jinsi alivyomupandisha Mordekayi cheo na kumupatia heshima kubwa, yote yameandikwa katika kitabu cha Mambo ya Siku cha ufalme wa Media na Persia.