Esther 10:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa na mkuu miongoni mwa Wayahudi. Aliheshimiwa sana na Wayahudi wenzake wengi, kwa sababu alifanya kazi kwa manufaa ya watu wake na kutetea ustawi wa Wayahudi wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahusuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, alipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Myuda Mordekai alikuwa wa pili kwake mfalme Ahaswerosi na mkuu kwa Wayuda, akapendwa na ndugu zake waliokuwa wengi, kwa kuwa aliwatakia mema walio ukoo wake, akasema nao wote walio wa kizazi chake maneno ya utengemano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mordekayi, Muyuda, alikuwa wa kwanza chini ya mufalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayuda, maana alitumika kwa faida na amani ya watu wake na wazao wao wote.