Esther 2:11 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila siku Mordekai alipitapita mbele ya ua wa nyumba hiyo ya wanawake ili apate kujua hali ya Esta na mambo ambayo yangempata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila siku Mordekai alikuwa akitembeatembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake kujua Esta alivyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na hayo yatakayompata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila siku Mordekai alipitapita mbele ya ua wa nyumba hiyo ya wanawake ili apate kujua hali ya Esta na mambo ambayo yangempata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila siku Mordekai alikuwa akitembea tembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake na masuria kuona jinsi Esta anavyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila siku Mordekai alikuwa akitembeatembea karibu na ua wa nyumba ya wanawake kujua Esta alivyoendelea na kuona yaliyokuwa yakitendeka kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mordekai akatembea siku kwa siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ajue, kama Esteri hajambo, tena ayajue nayo yatakayompata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na hayo yatakayompata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila siku Mordekayi alipitapita mbele ya kiwanja cha nyumba hiyo ya wanawake kusudi apate kujua hali ya Esteri na mambo ambayo yangemupata.