Esther 2:12 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kipindi cha hao wasichana kujiremba na kujitia uzuri kilichukua mwaka mmoja: Miezi sita ya kwanza walitumia mafuta ya manemane, na miezi sita ya mwisho walitumia manukato na mafuta mengineyo. Baada ya hapo, kila mwali, peke yake, alipelekwa kwa mfalme Ahasuero.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla zamu ya msichana haijafika ya kwenda kwa Mfalme Ahasuero, ilimbidi atimize miezi kumi na mbili ya matunzo ya urembo kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa miezi sita walikuwa wajipake mafuta ya manemane, na miezi sita kujipaka manukato na vipodozi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ilipowadia zamu yake mwanamwali mmojawapo aingie kwa mfalme Ahasuero, hali akiisha kufanyiwa sawasawa na sheria ya wanawake miezi kumi na miwili; yaani, ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kipindi cha hao wasichana kujiremba na kujitia uzuri kilichukua mwaka mmoja: miezi sita ya kwanza walitumia mafuta ya manemane, na miezi sita ya mwisho walitumia manukato na mafuta mengineyo. Baada ya hapo, kila mwali, peke yake, alipelekwa kwa mfalme Ahasuero.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla zamu ya msichana haijafika ya kwenda kwa Mfalme Ahusuero, ilimbidi atimize miezi kumi na miwili ya matunzo ya urembo kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa miezi sita walikuwa wajipake mafuta ya manemane na miezi sita ya kujipaka manukato na vipodozi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla zamu ya msichana haijafika ya kwenda kwa Mfalme Ahasuero, ilimbidi atimize miezi kumi na miwili ya matunzo ya urembo kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa miezi sita walikuwa wajipake mafuta ya manemane, na miezi sita kujipaka manukato na vipodozi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zilipotimia, hao vijana wakapelekwa mmoja mmoja kwa mfalme Ahaswerosi; vikafanyika, walipokwisha kukaa huko miezi kumi na miwili na kuyafuata maongozi ya wanawake. Kwani hapo ndipo, zilipotimia siku za kutakaswa kwao: miezi sita walipakwa kwa mafuta ya manemane, miezi sita mingine kwa manukato mengine, wanawake waliyoyatumia ya kutengenezea uzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ilipowadia zamu yake mwanamwali mmojawapo aingie kwa mfalme Ahasuero, hali akiisha kufanyiwa sawasawa na sheria ya wanawake miezi kumi na miwili; yaani, ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kipindi cha hao wabinti kwa kujipodoa na kujitia uzuri kilikuwa mwaka mumoja: miezi sita ya kwanza walitumia mafuta ya manemane, na miezi sita ya mwisho walitumia marasi na mafuta mengine. Nyuma ya pale, kila binti, peke yake, alipelekwa kwa mufalme Ahasuero.