Esther 2:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa kwenda kwa mfalme, kila mwali alipewa kila alichotaka kuchukua kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho ikulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi hivi ndivyo ambavyo msichana angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka nyumba ya wanawake na kwenda navyo katika jumba la mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila akitakacho hupewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa kwenda kwa mfalme, kila mwali alipewa kila alichotaka kuchukua kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho ikulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi hivi ndivyo ambavyo Esta angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka katika nyumba ya wanawake na masuria na kwenda navyo katika jumba la mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi hivi ndivyo ambavyo msichana angeingia kwa mfalme: Kila kitu alichohitaji aliruhusiwa kuchukua kutoka nyumba ya wanawake na kwenda navyo katika jumba la mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, hayo yalipokwisha, kila mara kijana alipoingia kwa mfalme hupewa yote, aliyoyataka kwenda nayo kutoka mle nyumbani mwa wanawake kuingia nyumbani mwa mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila akitakacho hupewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa kwenda kwa mufalme, kila binti alipewa kila kitu alichotaka kutwaa kutoka nyumba ya wanawake kwenda nacho katika nyumba ya kifalme.