Esther 2:14 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jioni ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubuhi, mwali huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya Shaashgazi, towashi msimamizi wa masuria wa mfalme. Mwali haikumpasa kurudi kwa mfalme, isipokuwa kama mfalme amependezwa naye kiasi cha kuagiza aitwe kwa jina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jioni angeenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme hadi apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huenda jioni, na asubuhi hurudi nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jioni ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubuhi, mwali huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya Shaashgazi, towashi msimamizi wa masuria wa mfalme. Mwali haikumpasa kurudi kwa mfalme, isipokuwa kama mfalme amependezwa naye kiasi cha kuagiza aitwe kwa jina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jioni angekwenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake na masuria katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme ambaye alikuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme mpaka apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jioni angekwenda pale na asubuhi kurudi sehemu nyingine ya nyumba ya wanawake katika utunzaji wa Shaashgazi, towashi wa mfalme ambaye alikuwa mkuu wa masuria. Hangeweza kurudi kwa mfalme mpaka apendezwe naye na kuagiza aitwe kwa jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huenda jioni, tena hurudi asubuhi kukaa katika nyumba ya pili ya wanawake mkononi mwa Sasagazi, mtumishi wa nyumbani mwa mfalme aliyewaangalia masuria; haingii tena kwa mfalme, isipokuwa mfalme amependezwa naye, akaagiza, aitwe kwa jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huenda jioni, na asubuhi hurudi nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Magaribi ulikuwa ndio wakati wa kwenda, na kesho yake asubui, binti huyo alipelekwa katika nyumba nyingine ya wanawake, chini ya uongozi wa Sasagazi, towashi musimamizi wa wahabara wa mufalme. Binti hakupaswa kurudi kwa mufalme, isipokuwa kama mufalme amependezwa naye, na aliitwa kwa jina.