Esther 2:15 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati uliwadia wa Esta kwenda kwa mfalme. Huyo, binti Abihaili, binamu ya Mordekai, na ambaye alilelewa na Mordekai, hakuomba chochote zaidi ya kile alichopangiwa na Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wa mfalme. Kila mtu aliyemwona Esta, alipendezwa naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, binti Abihaili, mjomba wake), Esta hakutaka vitu zaidi ya vile Hegai, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake, alikuwa amemshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati uliwadia wa Esta kwenda kwa mfalme. Huyo, binti Abihaili, binamu ya Mordekai, na ambaye alilelewa na Mordekai, hakuomba chochote zaidi ya kile alichopangiwa na Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wa mfalme. Kila mtu aliyemwona Esta, alipendezwa naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, naye ni binti wa Abihaili mjomba wake) Esta hakutaka vitu zaidi ya vile ambavyo Hegai towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake na masuria alivyokuwa ameshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zamu ya Esta ilipofika kwenda kwa mfalme (msichana ambaye Mordekai alikuwa amemlea, binti wa Abihaili mjomba wake), Esta hakutaka vitu zaidi ya vile ambavyo Hegai, towashi wa mfalme aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake alivyokuwa amemshauri. Naye Esta alipata kibali kwa kila mtu aliyemwona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, ikatimia hata siku yake Esteri, mwana wa Abihaili, mjomba wake Mordekai aliyemchukua, awe mwanawe. Alipoingia kwa mfalme hakutaka kitu, ni vile tu, Hegai, mtumishi wa nyumbani mwa mfalme aliyewaangalia wanawake, alivyomwambia, aende navyo. Naye Esteri alikuwa anawapendeza wote waliomwona kwa macho yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ukafika wa Esteri kwenda kwa mufalme. Huyo, binti wa marehemu Abihaili, binamu ya Mordekayi, na ambaye alilelewa na Mordekayi, hakuomba kitu chochote zaidi ya kile alichopangiwa na Hegayi, towashi mwangalizi wa wanawake wa mufalme. Esteri akapata kukubaliwa mbele ya kila mutu aliyemwona.