Esther 2:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme alipendezwa zaidi na Esta kuliko alivyopendezwa na wanawake wengine wote. Alipendwa sana kuliko wasichana wengine. Basi, mfalme akamvika taji ya kimalkia kichwani, akamfanya malkia badala ya Vashti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mfalme alivutiwa na Esta kuliko wanawake wengine wote, naye akapata upendeleo na kibali kuliko mabikira wengine. Kisha akamvika taji la kifalme kichwani mwake na kumfanya malkia badala ya Vashti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme alipendezwa zaidi na Esta kuliko alivyopendezwa na wanawake wengine wote. Alipendwa sana kuliko wasichana wengine. Basi, mfalme akamvika taji ya kimalkia kichwani, akamfanya malkia badala ya Vashti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikawa mfalme alivutiwa na Esta zaidi kuliko wanawake wengine wote, naye akapata upendeleo na kibali kuliko mabikira wengine. Kisha akamvika taji la kifalme kichwani mwake na kumfanya malkia badala ya Vashti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikawa mfalme alivutiwa na Esta kuliko wanawake wengine wote, naye akapata upendeleo na kibali kuliko mabikira wengine. Kisha akamvika taji la kifalme kichwani mwake na kumfanya malkia badala ya Vashti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akampenda Esteri kuliko wanawake wote, kwani aliona upendeleo na utu mbele yake kuliko wanawali wote, akamvika kilemba cha kifalme kichwani pake, akamweka kuwa mkewe mahali pa Wasti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamupenda zaidi Esteri kuliko wanawake wote. Naye Esteri akapata kukubaliwa na kutendewa mema mbele yake zaidi kuliko wabinti wengine wote. Basi, mufalme akamuvalisha taji ya kimalkia kwenye kichwa, akamufanya malkia pahali pa Vashiti.