Esther 2:20 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Esta alikuwa bado hajajitambulisha ukoo wala kabila lake kama Mordekai alivyokuwa amemwonya asifanye hivyo; naye Esta alimtii kama alivyokuwa akimtii wakati wa utoto wake, alipolelewa naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya asili yake na uraia wake, kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Esta alikuwa bado hajajitambulisha ukoo wala kabila lake kama Mordekai alivyokuwa amemwonya asifanye hivyo; naye Esta alimtii kama alivyokuwa akimtii wakati wa utoto wake, alipolelewa naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya kabila lake na uraia wake kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Esta alikuwa ameficha siri ya kabila lake na uraia wake, kama Mordekai alivyokuwa amemwambia, kwa maana aliendelea kufuata maelekezo ya Mordekai kama alivyokuwa akifanya alipokuwa akimlea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Esteri alikuwa hajaujulisha mlango wake wala ukoo wake, kama Mordekai alivyomwagiza; kwani Esteri aliyafanya maagizo yake Mordekai kama hapo, alipomlea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Esteri alikuwa bado hajatambulisha ukoo wala kabila lake kama vile Mordekayi alivyokuwa amemwonya asifanye. Naye Esteri akamutii kama alivyokuwa akimutii wakati wa utoto wake, alipolelewa naye.