Esther 2:21 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Mordekai alipokuwa anaketi penye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi, wawili baadhi ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa milango ya vyumba vya mfalme, waliudhika kiasi cha kula njama kumuua mfalme Ahasuero.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa Mordekai alipokuwa ameketi kwenye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi, maafisa wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa lango, walikasirika na kupanga njama ya kumuua Mfalme Ahasuero.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Mordekai alipokuwa anaketi penye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi, wawili baadhi ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa milango ya vyumba vya mfalme, waliudhika kiasi cha kula njama kumuua mfalme Ahasuero.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Mordekai alipokuwa ameketi kwenye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi maafisa wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa lango, walikasirika na kupanga njama ya kumwua Mfalme Ahusuero.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Mordekai alikuwa ameketi kwenye lango la mfalme, Bigthana na Tereshi, maafisa wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa lango, walikasirika na kupanga njama ya kumuua Mfalme Ahasuero.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile, Mordekai alipokaa langoni pa mfalme, watumishi wawili wa mfalme wa nyumbani waliokuwa walinda mlango, ndio Bigitana na Teresi, wakakasirika sana, wakatafuta njia ya kumwua mfalme Ahaswerosi kwa mikono yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Mordekayi alipokuwa anaikaa kwenye mulango wa mufalme, Bigitani na Teresi, wawili kati ya matowashi wa mufalme waliokuwa walinzi wa milango ya vyumba vya mufalme, walikasirika hata wakafanya shauri baya la kumwua mufalme Ahasuero.