Esther 2:22 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mordekai aliingamua njama hiyo, akamjulisha malkia Esta, naye Esta akampasha habari mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mordekai aligundua hila hii na kumwambia Malkia Esta, ambaye baadaye alimwarifu mfalme, huku akimsifu Mordekai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mordekai aliing'amua njama hiyo, akamjulisha malkia Esta, naye Esta akampasha habari mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mordekai aligundua juu ya hila hii na kumwambia Malkia Esta, ambaye baadaye alimwarifu mfalme huku akimsifu Mordekai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mordekai aligundua hila hii na kumwambia Malkia Esta, ambaye baadaye alimwarifu mfalme, huku akimsifu Mordekai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mordekai akapata kulijua shauri hilo, akamsimulia Esteri, mkewe mfalme, naye Esteri akamwambia mfalme katika jina la Mordekai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mordekayi akapata habari hiyo, akamujulisha malkia Esteri, naye Esteri akamupasha mufalme habari.