Esther 2:23 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uchunguzi ulipofanywa, iligunduliwa kuwa ni kweli; basi, watu hao wawili wakatundikwa kwenye mti wa kuulia. Habari kuhusu tukio hilo iliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Taarifa hiyo ilipochunguzwa na kuonekana kuwa kweli, maafisa hao wawili waliangikwa juu ya miti ya kunyongea. Haya yote yaliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jambo hilo lilipochunguzwa, na hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo pia yakaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uchunguzi ulipofanywa, iligunduliwa kuwa ni kweli; basi, watu hao wawili wakatundikwa kwenye mti wa kuulia. Habari kuhusu tukio hilo iliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakati taarifa hiyo ilipochunguzwa na kuonekana kuwa kweli, maafisa hao wawili waliangikwa juu ya miti ya kunyongea. Haya yote yaliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Taarifa hiyo ilipochunguzwa na kuonekana kuwa kweli, maafisa hao wawili waliangikwa juu ya miti ya kunyongea. Haya yote yaliandikwa katika kitabu cha kumbukumbu mbele ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha shauri hilo likanyatiwa, hata likavumbulikana, nao wale wawili wakatundikwa katika mti. Mambo haya yakaandikwa katika kitabu cha mambo ya siku machoni pa mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jambo hilo lilipochunguzwa, na hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo pia yakaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uchunguzi ulipofanywa, iligunduliwa kwamba ni kweli; basi, watu hao wawili wakatundikwa juu ya muti. Habari juu ya tukio hilo iliandikwa katika kitabu cha Mambo ya Siku mbele ya mufalme.