Esther 2:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unaweza kuteua maofisa katika kila mkoa wa utawala wako, na kuwaagiza wawalete wasichana wazuri wote kwenye nyumba ya wanawake hapa Susa, mji mkuu. Halafu wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wako; na hapo wapewe mafuta na vifaa vingine ili wajirembeshe zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme na awateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi wa mfalme, aliyekuwa msimamizi wa wanawake; na wapewe huduma zote za urembo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye mfalme aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Shushani ngomeni, kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi-wa-nyumba wa mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unaweza kuteua maofisa katika kila mkoa wa utawala wako, na kuwaagiza wawalete wasichana wazuri wote kwenye nyumba ya wanawake hapa Susa, mji mkuu. Halafu wawekwe chini ya uangalizi wa Hegai, towashi mwangalizi wa wanawake wako; na hapo wapewe mafuta na vifaa vingine ili wajirembeshe zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake na masuria katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya utunzaji wa Hegai, towashi wa mfalme, ambaye ndiye kiongozi wa wanawake, na wapewe matunzo yote ya urembo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme na ateue maafisa katika kila jimbo la himaya yake kuwaleta hao wanawali wote wazuri wa sura katika nyumba ya wanawake katika ngome ya mji wa Shushani. Kisha wawekwe chini ya utunzaji wa Hegai, towashi wa mfalme, msimamizi wa wanawake; na wapewe matunzo yote ya urembo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme na aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, wawakusanye vijana wa kike wote walio wanawali wenye sura nzuri, wawapeleke Susani jumbani mwa mfalme na kuwatia chumbani mwa wanawake mkononi mwake Hegai aliye mtumishi wa mfalme wa nyumbani wa kuwaangalia wanawake, kisha wapewe vyombo vyao vya kutengenezea uzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye mfalme aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Shushani ngomeni, kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi-wa-nyumba wa mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme achague wakubwa katika kila jimbo la utawala wake, na kuwaagiza wawalete wabinti wote wazuri ambao ni mabikira kwenye nyumba ya wanawake hapa Susani, muji mukubwa. Halafu wawekwe chini ya uangalizi wa Hegayi, towashi mwangalizi wa wanawake wako; na hapo wapewe mafuta na vifaa vingine kusudi wajipambe zaidi.