Esther 2:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Amri ya mfalme ilipotangazwa hadharani, wasichana wengi walipelekwa Susa, mji mkuu, wakawekwa chini ya ulinzi wa Hegai. Esta naye, alipelekwa kwenye ikulu ya mfalme, akawekwa chini ya uangalizi wa Hegai, yule mwangalizi wa wanawake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Agizo na amri ya mfalme ilipotangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa kwa Hegai, aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Amri ya mfalme ilipotangazwa hadharani, wasichana wengi walipelekwa Susa, mji mkuu, wakawekwa chini ya ulinzi wa Hegai. Esta naye, alipelekwa kwenye ikulu ya mfalme, akawekwa chini ya uangalizi wa Hegai, yule mwangalizi wa wanawake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati agizo na amri ya mfalme lilipotangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa Hegai, ambaye alikuwa mkuu wa nyumba ya wanawake na masuria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati agizo na amri ya mfalme lilitangazwa, wanawali wengi waliletwa kwenye ngome ya mji wa Shushani na kuwekwa chini ya uangalizi wa Hegai. Pia Esta alipelekwa katika jumba la mfalme na akakabidhiwa Hegai, aliyekuwa mkuu wa nyumba ya wanawake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, agizo la mfalme, aliloliamrisha, lilipotangazwa, vijana wengi wa kike wakakusanywa Susani, mlimokuwa na jumba la mfalme, wakatiwa mkononi mwake Hegai; ndipo, Esteri naye alipochukuliwa na kupelekwa nyumbani mwa mfalme, akatiwa mikononi mwa Hegai aliyewaangalia wanawake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amri ya mufalme ilipotangazwa, wabinti wengi wakapelekwa Susani, muji mukubwa, wakawekwa chini ya ulinzi wa Hegayi. Esteri naye, akapelekwa kwenye nyumba ya kifalme, akawekwa chini ya uangalizi wa Hegayi, yule mwangalizi wa wanawake.