Esther 2:9 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hegai alipendezwa na Esta hata kiasi cha kumpendelea. Bila kupoteza wakati, alimpa Esta mafuta na chakula maalumu. Isitoshe, alimhamishia mahali pazuri kabisa katika nyumba hiyo ya wanawake, akamteulia watumwa wa kike saba kutoka ikulu ya mfalme, wamhudumie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msichana huyu alimpendeza na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya urembo na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka jumba la kifalme, na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hegai alipendezwa na Esta hata kiasi cha kumpendelea. Bila kupoteza wakati, alimpa Esta mafuta na chakula maalumu. Isitoshe, alimhamishia mahali pazuri kabisa katika nyumba hiyo ya wanawake, akamteulia watumwa wa kike saba kutoka ikulu ya mfalme, wamhudumie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msichana huyu alimpendeza mfalme na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya uzuri na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka katika jumba la kifalme na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake na masuria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msichana huyu alimpendeza na kupata kibali mbele zake. Mara moja akaanza kumpa matunzo ya uzuri na chakula maalum. Alimpa Esta vijakazi saba waliochaguliwa kutoka jumba la kifalme, na kumhamishia yeye pamoja na vijakazi wake katika sehemu bora zaidi katika nyumba ya wanawake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwona kijana huyu kuwa mzuri, akampendeza sana, kwa hiyo akajihimiza kumpa vyombo vyake vya kutengenezea uzuri na posho yake; kisha akampa vijana wa kike saba waliochaguliwa nyumbani mwa mfalme, akamkalisha pamoja na hao vijana wake nyumbani mwa wanawake katika chumba kilichokuwa kizuri zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hegayi akapendezwa na Esteri hata kiasi cha kumupendelea. Bila kupoteza wakati, akamupa Esteri mafuta na chakula. Vilevile, akamuhamishia pahali pazuri kabisa katika nyumba hiyo ya wanawake, akamuchagulia wajakazi saba kutoka nyumba ya mufalme.