Esther 3:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya mambo hayo, mfalme Ahasuero alimpandisha cheo Hamani, akawa waziri mkuu. Hamani alikuwa mwanawe Hamedatha, na wa uzao wa Agagi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya matukio haya, Mfalme Ahasuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya mambo hayo, mfalme Ahasuero alimpandisha cheo Hamani, akawa waziri mkuu. Hamani alikuwa mwanawe Hamedatha, na wa uzao wa Agagi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya matukio haya, Mfalme Ahusuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya matukio haya, Mfalme Ahasuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baada ya mambo hayo mfalme Ahaswerosi akampa Hamani, mwana wa Hamedata wa Agagi, kuwa mkuu akimwinua na kukiweka kiti cha ukuu wake juu zaidi kuliko vyao wakuu wote waliokuwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya mambo hayo, mufalme Ahasuero akamupandisha Hamani cheo, akakuwa waziri mukubwa. Hamani alikuwa mwana wa Hamedata wa uzao wa Agagi.