Esther 3:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akaivua pete yake, ambayo ilitumiwa kupigia mhuri matangazo, akampa adui wa Wayahudi Hamani mwana wa Hamedatha wa uzao wa Agagi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akaivua pete yake, ambayo ilitumiwa kupigia mhuri matangazo, akampa adui wa Wayahudi Hamani mwana wa Hamedatha wa uzao wa Agagi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kwenye kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kwenye kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipoitoa pete yake yenye muhuri kidoleni pake, akampa Hamani, mwana wa Hamedata wa Agagi, aliyekuwa mpingani wao Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akaivua pete yake, ambayo ilitumiwa kwa kupiga muhuri juu ya matangazo, akamupa adui wa Wayuda Hamani mwana wa Hamedata wa uzao wa Agagi.