Esther 3:12 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, Hamani aliwaita makatibu wote wa mfalme, akawapa tangazo ambalo alitaka litafsiriwe kwa kila lugha na kila namna ya maandishi katika utawala huo, halafu nakala zisambazwe kwa watawala wote, wakuu wa mikoa yote, na viongozi wa makabila — kufuatana na lugha zinazotumika kwao. Tangazo hilo lilitolewa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kupigwa mhuri kwa pete yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahasuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, Hamani aliwaita makatibu wote wa mfalme, akawapa tangazo ambalo alitaka litafsiriwe kwa kila lugha na kila namna ya maandishi katika utawala huo, halafu nakala zisambazwe kwa watawala wote, wakuu wa mikoa yote, na viongozi wa makabila — kufuatana na lugha zinazotumika kwao. Tangazo hilo lilitolewa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kupigwa mhuri kwa pete yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahusuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahasuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha waandishi wa mfalme wakaitwa katika mwezi wa kwanza siku ya kumi na tatu; yote, Hamani aliyoyaagiza, yakaandikwa baruani kwa watawala nchi wa mfalme na kwa wenye amri wa kila jimbo moja na kwa wakuu wa kila kabila moja, kwa kila jimbo katika maandiko yao na kwa kila kabila katika msemo wa kwao. Hizo barua zikaandikwa katika jina la mfalme Ahaswerosi, zikatiwa muhuri kwa ile pete ya mfalme yenye muhuri,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, Hamani akawaita waandishi wote wa mufalme, akawapa tangazo ambalo alitaka litafsiriwe kwa kila luga na kila namna ya maandiko katika utawala ule, na halafu mifano ya barua isambazwe kwa watawala wote, wakubwa wa majimbo yote, na viongozi wa makabila – kufuatana na luga zinazotumika kwao. Tangazo hilo likatolewa kwa jina la mufalme Ahasuero, na kupigwa muhuri kwa pete yake.