Esther 3:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matarishi walizipeleka nyaraka hizo kwa kila mkoa katika utawala huo. Tangazo hilo lilisema kwamba kwa siku moja tu, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari, Wayahudi wote — vijana kwa wazee, wanawake kwa watoto, wote lazima wauawe, waangamizwe na kufutiliwa mbali, na mali zao zote zichukuliwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote, wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo, siku moja, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, na pia kuteka nyara vitu vyao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matarishi walizipeleka nyaraka hizo kwa kila mkoa katika utawala huo. Tangazo hilo lilisema kwamba kwa siku moja tu, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari, Wayahudi wote — vijana kwa wazee, wanawake kwa watoto, wote lazima wauawe, waangamizwe na kufutiliwa mbali, na mali zao zote zichukuliwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo kwa siku moja. Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, walipaswa pia kuteka nyara vitu vyao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote, wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo, siku moja, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, na pia kuteka nyara vitu vyao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha zikapewa wapiga mbio, wazipeleke katika majimbo yote ya mfalme kwamba: Siku hiyo moja ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, Wayuda wote pia, vijana na wazee, wachanga na wanawake, watoweshwe kwa kuuawa na kwa kuangamizwa, nazo mali zao zitekwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wajumbe wakazipeleka barua hizo kwa kila jimbo katika utawala ule. Tangazo hilo lilisema kwamba kwa siku moja tu, ni kusema siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili unaoitwa Adari, Wayuda wote – tangia kwa vijana mpaka wazee, wanawake na watoto, wote wauawe, waangamizwe na kuteketezwa kabisa, na mali zao zote zinyanganywe.