Esther 3:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa amri ya mfalme, tangazo hili lilitolewa katika mji mkuu wa Susa, nao matarishi wakalitangaza katika mikoa yote. Mfalme na Hamani walikaa chini kunywa wakati watu mjini Susa wanafadhaika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walienda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa amri ya mfalme, tangazo hili lilitolewa katika mji mkuu wa Susa, nao matarishi wakalitangaza katika mikoa yote. Mfalme na Hamani walikaa chini kunywa wakati watu mjini Susa wanafadhaika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walikwenda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuharakishwa na amri ya mfalme, matarishi walikwenda na andiko lilitolewa katika mji wa ngome ya Shushani. Mfalme na Hamani waliketi na kunywa, lakini mji wa Shushani ulifadhaika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wapiga mbio wakatoka upesi kwa lile neno la mfalme. Namo mjini mwa Susani, mlimokuwa na jumba la mfalme, ile amri ya mfalme ikatangazwa. Kisha mfalme na Hamani wakakaa, wanywe, lakini mji wa Susani ukawa umevurugika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa amri ya mufalme, tangazo hili lilitolewa katika muji mukubwa wa Susani, nao wajumbe wakalitangaza katika majimbo yote. Mufalme na Hamani wakaikaa chini kwa kunywa wakati watu katika muji wa Susani wanafazaika.