Esther 3:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme aliamuru maofisa wote wa serikali yake wamtii Hamani kwa kumwinamia na kumsujudia. Lakini Mordekai, hakumwinamia wala kumsujudia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wote wa mfalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. Lakini Mordekai hakumpigia magoti wala kumheshimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme aliamuru maofisa wote wa serikali yake wamtii Hamani kwa kumwinamia na kumsujudia. Lakini Mordekai, hakumwinamia wala kumsujudia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wote wa kifalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. Lakini Mordekai hakumpigia magoti wala kumheshimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wote wa mfalme waliokaa langoni mwa mfalme walipiga magoti na kumpa Hamani heshima, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru hili kuhusu Hamani. Lakini Mordekai hakumpigia magoti wala kumheshimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo watumishi wote wa mfalme waliokuwako kule langoni kwa mfalme wakampigia Hamani magoti na kumwangukia, kwani hivyo ndivyo, mfalme alivyoagiza kwa ajili yake. Lakini Mordekai hakumpigia magoti, wala hakumwangukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akaamuru wakubwa wote wa serikali yake wamutii Hamani kwa kuinama na kupiga magoti mbele yake. Lakini Mordekayi hakuinama wala kupiga magoti mbele yake.